Nenda kwa yaliyomo

Zimbabwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Zimbabwe
Republic of Zimbabwe
Kaulimbiu: "Unity, Freedom, Work" (Kiingereza kwa "Umoja, Uhuru, Kazi")
Wimbo wa taifa: "Blessed be the Land of Zimbabwe"
Eneo la Zimbabwe
Mji mkuu
na mkubwa
Harare
Lugha rasmiKiingereza, Kishona, Sindebele
Kabila (2023)99.4% Waafrika
0.2% Wazungu
0.4% Wengine
SerikaliJamhuri ya rais wa umoja
 • Rais
Emmerson Mnangagwa
 • Makamu wa Rais
Constantino Chiwenga
Uhuru kutoka Uingereza
 • Uhuru kutoka Uingereza
18 Aprili 1980
 • Tangazo la Jamhuri
18 Aprili 1980
Eneo
 • Jumlakm2 390,757 km² (ya 60)
 • Maji (asilimia)1%
Idadi ya watu
 • Kadirio la 202416,868,409
 • Msongamano39/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2023
 • Jumla $44.448 bilioni (ya 131)
 • Kwa kila mtu $2,749(ya )
PLT (Kawaida)Kadirio la 2023
 • Jumla $32.424 bilioni
 • Kwa kila mtu $2,005
HDI (2022)decrease 0.550 kati
Gini (2019) 50.3
SarafuDola ya Zimbabwe (ZWL), Dola ya Marekani (USD)
Majira ya saaUTC+2 CAT
Upande wa magariKushoto
Msimbo wa simu+263
Jina la kikoa.zw

Zimbabwe, rasmi kama Jamhuri ya Zimbabwe, ni nchi inayopatikana katika Afrika ya Kusini, bila pwani, inayopakana na Zambia kaskazini, Msumbiji mashariki, Afrika Kusini kusini, na Botswana magharibi. Ina idadi ya watu takriban milioni 16.7, ikiwa ya 73 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Harare. Zimbabwe imegawanyika katika majimbo 10. Inajulikana kwa historia yake ya ustaarabu wa kale, hasa mji wa mawe wa Zimbabwe Kuu, maporomoko maarufu ya Victoria Falls, na historia yake ya kisiasa, ikiwemo utawala wa muda mrefu wa Robert Mugabe na changamoto za kiuchumi zilizoshuhudiwa katika karne ya 21.

Jina

Jina Zimbabwe linatokana na neno "dzimba dzamabwe" linalomaanisha "nyumba ya mawe" kwa lugha ya Kishona. Nyumba hiyo ya mawe, ambayo imehifadhiwa kama eneo la kihistoria, ilikuwa makao ya Ufalme wa Mutapa ambaye mfalme wake aliongoza eneo hilo miaka ya kale.

Mikoa ya Zimbabwe.
Pesa ya Zimbabwe hadi 2015, dollar ya Zimbabwe ilipofutwa, na Dolar ya Marekani kufanywa pesa rasmi.

Eneo

Zimbabwe imegawiwa katika mikoa 8 na miji 2 yenye hadhi ya mikoa. Imegawiwa zaidi katika wilaya 59 na kata 1,200.

Mikoa ya Zimbabwe ni:

Miji minne mikubwa ya Zimbabwe ni:

Maporomoko ya maji (Bridal Vei), paa za mashariki
Duka, Paa za mashariki, 1989

Historia

Historia ya awali

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Tangu karne ya 11, Zimbabwe ya leo imekuwa na falme imara kwenye njia muhimu ya biashara, hasa ufalme wa Mutapa.

Ukoloni

Kampuni ya British South Africa ya Cecil Rhodes iliweka mipaka ya sasa katika miaka ya 1890.

Koloni la Uingereza lilianzishwa mwaka 1923 kwa jina la Southern Rhodesia.

Mwaka 1965, serikali ya walowezi Wazungu ilijitangazia uhuru kwa jina la Rhodesia tu.

Baada ya miaka 14 ya kutengwa kimataifa na kupigana na raia Waafrika katika miaka ya 1970, mapatano ya mwaka 1979 yalikubali wakazi wote wawe na haki ya kupiga kura na nchi ikawa huru kweli kwa jina la Zimbabwe mwaka 1980.

Baada ya uhuru

Rais Robert Mugabe alipata umaarufu katika siasa kama mpiganaji dhidi ya ukoloni lakini pia kama aina ya dikteta aliyerudisha nyuma uchumi wa nchi.

Baada ya yeye kulazimishwa na wanajeshi kujiuzulu, tarehe 24 Novemba 2017 Emmerson Mnangagwa amekuwa rais mpya wa Zimbabwe.

Demografia

Kabila

Wakazi wengi (82%) ni wa kabila la Washona, 14% ni Wandebele, 2% ni wa makabila mengine ya Kiafrika, 1% ni machotara, Wahindi, Wazungu n.k.

Lugha

Kwa sasa lugha rasmi ni 16. Lugha kubwa ni Kishona (70%) na Kindebele (20%). Kiingereza ni lugha ya kwanza ya chini ya asilimia 2.5% za wakazi.

Dini

Upande wa dini, 84.1% ni Wakristo (hasa Waanglikana, Wakatoliki 8%, Wasabato na Wamethodisti). Waliobaki ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika (4.5%), ni Waislamu (0.7%), au hawana dini (10.2%) .

Tazama pia

Tanbihi


Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Serikali

Habari

Wanamgambo

Maelekezo

Utalii

Nyingine


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Zimbabwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.